Akatwa mguu kisa mapenzi
#MsasaUpdate AKATWA MGUU KWA SABABU YA MAPENZI
Kutoka kata ya Madilu, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Kijana aitwae Benard Mkolwe amepigwa na kuvunjwa mikono na miguu baada ya kukutwa akiwa na Sarah Mgohole (18) nyumbani kwao ambako alimfuata kwa lengo la kufanya mapenzi ikiwa ni siku yao ya kwanza tangu waanze uhusiano wiki mbili zilizopita.
Kijana huyo amekiri kuwa na uhusiano na Msichana huyo ambaye sio Mke wa Mtu na wala hasomi na kudai kuwa mapenzi yao yalikuwa ya kuwasiliana kwa simu pekee na yana muda wa wiki mbili toka wayaanzishe ambapo siku ya tukio hilo ilikuwa ni siku yao ya kwanza kukutana kwa lengo la kufanya mapenzi.
"Waliofanya tukio ni Baba zake wadogo wa yule Msichana yule Msichana na sijawahi kufanya kitu chochote kile tulikuwa ni marafiki wa kuchati na ile siku alivoniita nahisi ndio ilikuwa siku ya kuelekea kwenye tendo lakini sikufanya kitu chochote" Benard Mkolwe
Kwa sasa Mkolwe anatibiwa katika hospitali ya St. John's ambapo Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kupinga vikali vitendo vya Wananchi kujichukulia sheria mkononi
"Labda kuna visa vya awali,huu ni ukatili wa kijinsia unaotokana na binti kusuka mpango kumuonea huyu kijana, yeye amekubali kuchati halafu wanakuja kumpiga na kama alikuwa hana uhitaji wa kukutana na huyu kijana angemkatalia toka mwanzo" - DC Tsere."
Source: Millard Ayo.
Kwa habari kemkem za kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha tembelea Msasa Online kila wakati hakika hutopitwa na chochote saa 24.
Comments
Post a Comment