Sio kila spishi ina uwezo wa kucheka.

Sokwe wanaweza kucheka. Wanasayansi hata wameza kubaini sauti kama ya kucheka kutoka kwa panya kwa kuwatekenya.

Lakini ni binadamu na nyani wengine ambao wanachukuliwa kuwa pekee wenye uwezo wa kujibu kitu wanachokiona kwa kucheka.

Ingawa ni ishara ya kuwa na wakati mzuri wa zamani, kucheka vizuri ni mojawapo ya mambo magumu zaidi ambayo miili yetu hutoa. Hii ndio sababu.

Yote huanzia kwenye ubongo

Hatuchagui kucheka.

Hata kama umelipa ili kutazama vichekesho kutoka kwa mcheshi unayempenda, kwa hakika tunacheza kamari.

Ikiwa tutacheka kwa mzaha wakati wa onesho, sio hiari, ni kulingana na jinsi ubongo wetu huchakata kile tunachoona na kusikia.

Ni vigumu sana kuigiza kucheka au kulazimisha kucheka - jaribu mwenyewe. Haisikiki kuwa ya kweli, sivyo?

Comments